Mchezo dhidi ya Mwadui ni kufa au kupona

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Sep 2018
Mchezo dhidi ya Mwadui ni kufa au kupona
Simba inatarajiwa kuondoka leo mkoani Mwanza kwenda Shinyanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa sita dhidi ya Mwadui FC.

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye dimba la Kambarage.

Simba imeambulia alama moja pekee kwenye michezo yake miwili dhidi ya Ndanda FC na Mbao FC.

Ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na Ndanda na hapo jana ikakubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbao FC.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anahitaji kushinda mchezo huo ili kurejesha utulivu Msimbazi kwani matokeo tofauti yatakoleza moto ambao tayari moshi unafukuta.

Aussems anahitaji kufanyia kazi tatizo la umaliziaji kwa washambuliaji wake kwani Simba imekuwa ikicheza vizuri kwa muda wote na kutengeneza nafasi nyingi isipokuwa haifungi.

Simba ikiwa imeshuka dimbani mara nne imefunga mabao matatu pekee ambayo yote yamefungwa na Meddie Kagere.

Mabao hayo ni machache sana ukilinganisha na idadi kubwa ya nafasi zinazotengenezwa na Simba katika kila mchezo.

Simba haina kawaida ya kuwavumilia makocha pale timu inapofanya vibaya hivyo haitashangaza kama mchezo dhidi ya Mwadui FC ukawa wa mwisho kwa kocha Patrick Aussems kama Simba itashindwa kuibuka na ushindi.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba wanaotaka kocha huyo raia wa Ubelgiji atimuliwe na nafasi yake ichukuliwe na Masudi Djuma ambaye anaaminiwa sana na mashabiki.

Djuma ndiye aliyeiongoza Simba msimu uliopita baada ya kutimuliwa kwa kocha Joseph Omog kabla ya kuwasili Pierre Lechantre.

Akitumia mfumo wa 3-5-2, Simba ilifanikiwa kushinda michezo yote ya ligi chini yake huku pia ikifunga idadi kubwa ya mabao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’