Niyonzima ahofia kupoteza nafasi kikosi cha Rwanda kama hachezeshwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Sep 2018
Niyonzima ahofia kupoteza nafasi kikosi cha Rwanda kama hachezeshwi
Wakati Kocha Mkuu wake, Patrick Aussems akitangaza kumpa siku 14 ili awe fiti kabla ya kuanza kumtumia, kiungo wa kimataifa wa Simba, Haruna Niyonzima alisema ana mechi tano tu ndani ya Msimbazi kabla ya kuondoka.

Niyonzima alisema kama benchi la ufundi la Simba litaendelea kutomchezesha, basi atakuwa tayari kuvunja mkataba ili kulinda heshima anayopewa na Taifa lake la Rwanda.

Katika mahojiano na Mwanaspoti, Niyonzima alisema haumizwi na tatizo la kukosa namba katika kikosi cha Simba kwani uwezo anao na anajiamini lakini kikubwa anachokiomba ni kumpa heshima ili kumlindia namba katika kikosi cha Amavubi.

Alisema yupo fiti na ana uwezo wa kucheza Simba, ila suala la kupangwa au kutopangwa anamuachia kocha na kuweka wazi anaheshimu mipango yake.

β€œKupata kwangu nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba kinalinda heshima pia kinaniongezea uimara kuelekea michezo yetu iliyobaki atika kuwania nafasi ya kucheza fainali za Afcon 2019,” alisema.

Niyonzima alisema anaendelea vizuri na programu ya Kocha msaidizi Masoud Djuma na anaamini siku akipata nafasi ya kuitumikia timu yake atafanya mambo makubwa yatakayorudisha wapenzi wake wenye kiu ya kumuona akicheza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’