Huu utaratibu wa kuwashambulia viongozi, wachezaji na makocha baada ya kufungwa haufai

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Sep 2018
Huu utaratibu wa kuwashambulia viongozi, wachezaji na makocha baada ya kufungwa haufai
Jana Simba imefunga bao 1-0 na Mbao FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa dimba la CCM Kirumba.

Matokeo hayo hayakufurahiwa na kila mmoja wetu kwani haikuwa malengo ya timu kwenda kufungwa. Yemekuwa ni matokeo tu ya mchezo.

Mpira wa miguu una matokeo matatu yaani kushinda, kufungwa na pia kutoka sare. Lolote linaweza kutokea kwani hakuna timu ambayo imeandikiwa kushinda michezo yote.

Lakini jambo la kusikitisha ni kwa baadhi ya mashabiki wa Simba ambao jana waliwafanyia vurugu viongozi, makocha na wachezaji baada ya kupoteza mchezo.

Wapo mashabiki waliodiriki kuwarushia mawe na chupa wachezaji na kocha Patrick Aussems wakati wanatoka uwanjani.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara yeye alikuwa kwenye wakati mgumu zaidi kwani alishambuliwa uwanjani kwa kurushiwa chupa lakini pia ameendelea kushambuliwa kwa matusi kwenye mitandao ya kijamii.

Huu sio ustaarabu na ni vyema Wana Msimbazi tutakubaliana kuwa utamaduni huu haufai hata kidogo.

Matokeo ya jana wamemuuma kila mmoja, tufuate njia sahihi kuonyesha hasira zetu na sio kuwashambulia (kwa silaha) viongozi na wachezaji wa Simba.

Tukio lile la kuwapiga na chupa wachezaji linaweza kuwafanya washuke morali kwani ilipaswa waungwe mkono katika nyakati zote.

Tuwapongeze wakifanya vizuri lakini pia tuwaunge mkono na tuwatie moyo pale wanapofanya vibaya. Upendo utawafanya wajihisi wana deni kubwa kwa mashabiki wao.

Lakini chuki itawafanya wajihisi hawathaminiwi na kuacha kuipigania timu kwa moyo wote.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
19h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’