Uongozi wa klabu ya Simba umewaomba radhi wanachama na mashabiki wake baada ya kupoteza mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC leo.
Mkuu wa habari wa klabu ya SImba Haji Manara amesema matokeo hayo yamewaumiza wao viongozi pia na wameahidi kuchukua hatua pasipo presha.
"Bodi ya Wakurugenzi,Sekretarieti,Benchi la Ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba,wanawaomba radhi Wanachama na Washabiki wetu kwa matokeo ya leo.
"Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu. Tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi MAKUBWA ya Timu na klabu.
"Nawaomba mtulie katika kipindi hiki," amesema Manara.
Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba ambao hawaridhishwi na uwezo wa kocha Mkuu Patrick Aussems ambaye ndio kwanza ametimiza miezi miwili tangu aanze kuinoa Simba.

ADVERTISE HERE