Aussems apania kuondoka na alama tatu Mwanza

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Sep 2018
Aussems apania kuondoka na alama tatu Mwanza
Simba inashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba leo kuikabili Mbao FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Kwenye mchezo huo Simba itawakosa Asante Kwasi, Mzamiru Yassin na Hassan Dilunga kutokana na sababu za ugonjwa na majeruhi.

Haruna Niyonzima na Juuko Murshidi wao wameanza mazoezi mwanzoni mwa wiki hii hivyo hawakusafiri na kikosi cha Simba kilichotua Mwanza juzi.

Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kuwa maandalizi yamekamilika na atapambana kuhakikisha anapata matokeo kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambao aliutumia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na kuibuka na ushindi dhidi ya Mtibwa.

β€œNi mechi ngumu ambayo tunahitaji kupambana kuweza kupata ushindi kwa upande wa uwanja ni changamoto lakini tumewahi kuutumia uwanja huu kwenye mechi ya Ngao ya Jamii hivyo tunaujua.

β€œWachezaji wapo fiti kupambana na lengo ni kupata pointi tatu muhimu na kusonga mbele na tunaenda kwa tahadhari kubwa sababu tunawaheshimu wapinzani wetu hivyo tunaenda kupambana,” alisema Aussmes.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’