Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kiko tayari kuikabili Mbao FC kwenye mchezo wa ligi Kuu ya Tanzania Bara unaopigwa leo Alhamisi kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Simba iko mkoani Mwanza tangu juzi ambapo jana jioni ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye dimba la CCM Kirumba tayari kwa mchezo huo.
Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba Haji Manara yuko jijini Mwanza amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu. Mchezo wa leo tunajua hautakuwa mwepesi lakini tumejipanga kuondoka na alama zote tatu."
"Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kwenye uwanja wa CCM Kirumba waje kutuunga mkono," amesema Manara.
Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Ndanda FC kwenye mchezo uliopita, Simba inahitaji kushinda mchezo wa leo ili kutuliza 'mzuka' wa mashabiki wake ambao hawafurahishwi na mwenendo wa timu chini ya kocha Mkuu Patrick Aussems.
Matokeo yoyote tofauti na ushindi leo yataongeza presha kwa Aussems ambaye analaumiwa kwa kutomtumia Kocha Msaidizi Masudi Djuma ambaye ana uzoefu wa michezo ya mikoani.
Djuma ameachwa jijini Dar es salaam akiendelea kukinoa kikosi cha pili cha Simba kinachojumuisha wachezaji ambao hawakusafiri.
Hii ni mara ya pili kwa Djuma kuachwa Dar kwani pia hakusafiri na timu mkoani Mtwawa.

ADVERTISE HERE