Mkuu wa Habari wa Simba Haji Manara amesema timu hiyo bado haijapokea taarifa rasmi kutoka TFF ya kuwataka wasitishe mchakato wao wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 03, 2018.
Kwa sababu hiyo Manara amesema wataendelea na mchakato wa uchaguzi kama ulivyopangwa.
Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi (TFF), Revocatus Kuuli, alitangaza kusitishwa kwa mchakato huo akieleza kuwa umegubikwa na mambo mengi ambayo hayajafuata taratibu rasmi.
"Bado hatujapokea taarifa rasmi kutoka TFF inayotutaka tusitishe mchakato wa uchaguzi. Sasa kwa kuwa hiyo taarifa hatujaipokea, sisi tunaendelea," amesema Manara.

ADVERTISE HERE