Simba itajuta kumuacha Djuma michezo ya mikoani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Sep 2018
Simba itajuta kumuacha Djuma michezo ya mikoani
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alimwacha msaidizi wake, Masoud Djuma katika safari ya Mtwara walipocheza na Ndanda FC, lakini walichokutana nacho huko ni suluhu iliyowaibua wadau wengi wa soka.

Wadau hao wanasema, Djuma ambae aliachwa Dar es Salaam kwa programu maalumu na baadhi ya wachezaji ni sababu ya Simba kupata matokeo hayo.

Hii ni kwa sababu, Aussems hana uzoefu na mikoa ya Tanzania na namna ambavyo wanazicheza mechi za namna hiyo.

Mchambuzi makini wa soka, Ally Mayai amesema: β€œDjuma anazijua timu kuliko Aussems, lakini pia hata mechi za mikoani anazijua vizuri namna ya kuzicheza."

Amesema, Djuma ni muhimu kwenye timu kwa sababu aliweza kukaa mwenyewe katika benchi akiongoza Simba na kutengeneza mfumo wake wa 3-5-2, ambao ulifanikiwa na kuchukua ubingwa.

"Kukosekana kwake kwenye timu, inaweza ikawa sababu kubwa iliyochangia wakapata matokeo hayo yaliyowapa pointi moja,” alisisitiza Mayai mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.

Mayai aliongeza na kusema, Aussems pia, alikosea kutumia mfumo wa kuwacheza washambuliaji watatu wakati uwanja haukuwa rafiki kwake katika kufanya mashambulizi.

Kumekuwa na siri kubwa kati ya Djuma na uongozi wa Simba ikielezwa huenda Simba inataka kuachana na Djuma.

Wadau wametahadharisha kuwa Simba itafanya kosa kubwa sana kama itamuacha Djuma.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’