Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinatarajiwa kusafiri Novemba 9 kuelekea Benin kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya taifa hilo linaloshika nafasi ya 79 kwenye ubora wa viwango vya soka huku Stars ikiwa ya 136.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema atautumia mchezo huo utakaochezwa Novemba 12 kama kipimo halisi kwa vijana wake kabla ya kuendelea na harakati za kupigania tiketi ya kushiriki mashindano ya mataifa ya Afrika 2019, Cameroon.
"Hatujawa na michezo mikubwa hivi karibuni kwenye kalenda ya kimataifa ya FIFA, hilo limetufanya kushindwa hata kufanya vizuri kwenye ile orodha ya viwango vya ubora wa soka Duniani ambavyo hutolewa kila mwezi," alisema kocha huyo.
Mchezo huo wa kirafiki unategemewa kuchezwa kwenye uwanja wa Stade de l'Amitie (Cotonou) wenye uwezo wa kuingiza watazamaji wapatao 20,000.

ADVERTISE HERE