Kikosi cha Mabingwa wa Tanzania Bara Simba kesho Jumamosi, Septemba 15 2018 kinashuka kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kuikabili Ndanda FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Simba iko mkoani Mtwara tangu jana Alhamisi ikiwa na silaha zake zote ambapo leo ilifanya mazoezi kwenye uwanja huo kuelekea mchezo wa kesho.
Kocha wa Simba Patrick Aussems anatarajiwa kushusha kikosi chake kamili kinachowajumuisha washambuliaji wake wote John Bocco, Emanuel Okwi na Meddie Kagere.
Kagere ndiye kinara wa mabao kwenye ligi akiwa tayari ametupia nyavuni mabao matatu katika michezo miwili aliyoitumikia Simba.
Kiungo Mzambia Cletus Chama naye anatarajiwa kuanza kuitumikia Simba kwa mara ya kwanza kwenye ligi baada ya kupata ITC.

ADVERTISE HERE