Kilichoongezwa kwenye toleo jipya la Mwana Msimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Sep 2018
Kilichoongezwa kwenye toleo jipya la Mwana Msimbazi
Toleo la Mwana Msimbazi namba 1.1.9 limewekwa Play Store ambapo tofauti na zamani, kwa sasa ni lazima kuwa na toleo linalokwenda na wakati ili kuendelea kuhabarika.

Kila toleo linakuwa na maboresho yake muhimu na ni hivyo hivyo kwa toleo namba 1.1.9

SASA UNAWEZA KUONDOA MATANGAZO

Uwepo wa matangazo kwenye App ni moja ya njia zinazoiwezesha Mwana Msimbazi kuendelea kuwa hewani kwani kiasi kidogo cha malipo yanayopatikana katika matangazo hayo kinasaidia katika gharama za uendeshaji.

Lakini sasa toleo jipya limempa mtumiaji uwezo wa kuondoa matangazo hayo kwa MWAKA MZIMA kwa anayehitaji kwa kujiunga kupitia PLAY STORE.

Hivi karibuni kampuni ya Google inayomiliki PLAY STORE iliingia mkataba na kampuni za Mawasiliano za TIGO na VODACOM kuwawezesha watumiaji kupata huduma za kulipia zinazopatikana katika PLAY STORE.

Sasa unaweza kuondoa matangazo kwenye App yako MWAKA MZIMA kwa kujiunga na huduma hiyo kwa kulipia Tsh 2,200/- tu.

JINSI YA KUJIUNGA

Fungua ukurasa wa pembeni wa App yako, Bonyeza ONDOA MATANGAZO halafu fuata maelekezo yanayotolewa na PLAY STORE.



Kwa watumiaji wa Mtandao wa TIGO wanaweza kujiunga kupitia TIGOPESA wakati kwa wale wa VODACOM wanaweza kulipia huduma hiyo kupitia SALIO la simu.

Pia Vodacom kwa ushirikiano na kampuni ya MasterCard pamoja na benki ya BancABC wamezindua huduma inayomuwezesha mtumiaji yeyote wa huduma ya MPesa kuweza kutengeneza kadi ya MasterCard kwa njia ya M-Pesa na muda huo huo kuweza kuhamishia pesa kwenda akaunti hiyo na kisha kuweza kuanza kuitumia mara moja kufanya manunuzi mtandaoni.

Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wa mitandao ya TIGO na MPESA.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’