Bendera ya Tanzania kwenye mikono salama ya Mnyama leo dhidi ya Orlando Pirates

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Bendera ya Tanzania kwenye mikono salama ya Mnyama leo dhidi ya Orlando Pirates

Macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini leo yataelekezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambako Simba SC itashuka dimbani kuikabili Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Pambano hilo la Kundi C litapigwa kuanzia saa 10:00 jioni, huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa na jukumu la kulinda heshima ya soka la Tanzania katika michuano ya kimataifa.

Baada ya watani zao, Yanga SC, kuangukia pua kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya MC Alger kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, huku Azam FC nao wakichapwa mabao 2-1 na Al Ahli Tripoli juzi kwenye dimba hilo hilo kwenye kombe la Shirikisho, matumaini ya ushindi kwa wawakilishi wa Tanzania sasa yapo kwa Mnyama.

Bendera ya Tanzania ipo mabegani mwa vijana wa kocha Steve Barker, ambao leo wana jukumu la kuhakikisha furaha ya Wanasimba na mashabiki wa soka nchini inalindwa kwa gharama yoyote.

Vita ya Vinara

Hautakuwa mchezo mwepesi kutokana na ukweli kwamba zinakutana timu mbili ambazo zimeonyesha uimara mkubwa tangu kuanza kwa msimu huu.

Simba na Orlando Pirates ni vinara wa ligi katika nchi zao, huku kila mmoja akiwa bado hajaonja ladha ya kipigo kwenye ligi ya ndani.

Mnyama ameshinda michezo yote 11 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati Orlando Pirates wameshinda michezo tisa na kutoka sare mchezo mmoja katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Takwimu hizo zinatoa picha ya ukubwa wa pambano la leo, lakini Simba ina faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wake ambao wanatarajiwa kuligeuza dimba la Uhuru kuwa tanuri la moto kwa wageni wao.

Alama tatu ni lazima

Baada ya RS Berkane ya Morocco kuifumua Colombe ya Cameroon kwa mabao 4-1 hapo jana na kujiweka kileleni mwa msimamo wa Kundi C, Simba haina budi kuhakikisha inapata ushindi katika mchezo wa leo.

Ushindi huo utakuwa muhimu katika kuhakikisha mkakati wa Mnyama wa kuvuna alama zote tisa katika michezo yake mitatu ya nyumbani unabaki salama, sambamba na dhamira yake ya kuongoza kundi hilo.

Simba imeweka wazi malengo yake ya kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo msimu huu, na safari ya kutimiza ndoto hiyo inaanzia kwenye dimba la Uhuru leo.

Baada ya wiki moja ya kuandaa dozi kambini, sasa ni wakati wa vijana wa Barker kuzungumza kwa vitendo ndani ya dakika 90.

Leo si suala la Simba pekee, bali ni suala la heshima ya soka la Tanzania. Mnyama ana nafasi ya kurejesha tabasamu kwa mashabiki wa soka nchini na kuhakikisha bendera ya Tanzania inaendelea kupepea kwa fahari katika anga la soka la Afrika.

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 29 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Tumeweka malengo ya kufanya vizuri msimu huu – Maema
Tumeweka malengo ya kufanya vizuri msimu huu – Maema
17h ago
READ MORE β†’
Barker apania ushindi dhidi ya Orlando Pirates
Barker apania ushindi dhidi ya Orlando Pirates
17h ago
READ MORE β†’
Simba vs Pirates, dozi inakamilishwa leo
Simba vs Pirates, dozi inakamilishwa leo
1d ago
READ MORE β†’
Today's Newspapers, Saturday, November 28th, 2026
Today's Newspapers, Saturday, November 28th, 2026
1d ago
READ MORE β†’
Wagombea 40 wavuka mchujo wa awali Simba, Mangungu na Julio watemwa
Wagombea 40 wavuka mchujo wa awali Simba, Mangungu na Julio watemwa
1d ago
READ MORE β†’
Tuanze kuisaka robo fainali kwa ushindi dhidi ya Orlando Pirates - Ahmed Ali
Tuanze kuisaka robo fainali kwa ushindi dhidi ya Orlando Pirates - Ahmed Ali
1d ago
READ MORE β†’
Toure tayari kurejea dhidi ya Pirates
Toure tayari kurejea dhidi ya Pirates
1d ago
READ MORE β†’
Semaji awatisha Orlando Pirates 'watake, wasitake watapasuka'
Semaji awatisha Orlando Pirates 'watake, wasitake watapasuka'
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
2d ago
READ MORE β†’