KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza orodha ya awali ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Klabu ya Simba SC, huku wanane kati ya 48 waliorejesha fomu wakikosekana kwenye orodha hiyo.
Katika orodha iliyotolewa leo, Ijumaa, Novemba 27, 2026, wagombea wanne wamefanikiwa kuvuka mchujo wa awali katika nafasi ya Mwenyekiti, huku wengine 36 wakisonga mbele katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
Jina kubwa lililokosekana katika mbio za Uenyekiti ni la Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Murtaza Ally Mangungu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama saba waliorejesha fomu za kuwania nafasi hiyo.
Wengine ambao hawapo kwenye orodha mpya ya wanaowania Uenyekiti ni Mohamed Khamis Soloka na Selemani Haroub Said.
Kwa upande wa Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio', ni miongoni mwa watano ambao majina yao hayapo kwenye orodha iliyotangazwa baada ya mchujo.
Wengine ni Andrew Julius Tupa, Mariam Mussa Shemzigwa, Omari Juma Mazola na Pendo Aidan Mapugio.
Hata hivyo, katika taarifa hiyo, Kamati ya Uchaguzi haijaeleza sababu za kila mmoja wa wagombea hao kukosekana kwenye orodha mpya.
WAGOMBEA WALIOVUKA MCHUJO WA AWALI
Nafasi ya Mwenyekiti (4)
-
Anindumi Jonas Semu
-
Geofrey Irick Nyange
-
Dkt. Seif Ramadhani Muba
-
Swedy Khamis Mkwabi
Nafasi ya Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi (36)
-
Aaron Henry Mrina
-
Abdallah Rashid Mgomba
-
Alfred Martin Elia
-
Arnold Nzuamtemi Nzali
-
Aziza Hussein Kaku
-
Christopher Kabalika Mwansasu
-
Damian Samweli Manembe
-
Eli Achahofu Paulo
-
Enock Bwigane Mwasubila
-
Fadhili Mohamed Famonga
-
Farid Awadh Tamim
-
Francis Kumba Ndulane
-
Hamisi Omari Tika
-
Hassan Bakari Kakayoo
-
Hussein Ally Simba
-
Isabella Samwel Faya
-
Issa Masoud
-
Jonathan Wilisaa Nkya
-
Juma Abbas Pinto
-
Laurian Salvatory Mganga
-
Mariam Abdallah Ibrahim
-
Muhamadi Mohamedi Hamisi
-
Rachel Juma Chagonja
-
Raphael Masunga Chegeni
-
Richard Shukia
-
Rodney Makamba Chiduo
-
Said Hassan Tulliy
-
Saidi Abdallah Njechele
-
Saleh Mohamed Afif
-
Salum Issaka Hamidu
-
Salum Kassim Maftah
-
Shukuru Athumani Mtego
-
Dkt. Suleiman Serera
-
Ussi Salum Pondeza
-
Wilfred Elias Nyamwija
-
Yusuph Omary Yenga
ZAMU YA MAPINGAMIZI
Licha ya wagombea hao 40 kuvuka hatua ya kwanza, safari yao kuelekea kwenye uchaguzi bado haijakamilika, kwani sasa wanakwenda kukabiliwa na hatua nyingine ya mapingamizi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF, mapingamizi yataanza kupokelewa kuanzia kesho, Jumamosi, Novemba 28 hadi Jumapili, Novemba 29, 2026, kupitia barua pepe ya tanfootball@tff.or.tz.