Toure tayari kurejea dhidi ya Pirates

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
13m ago
Toure tayari kurejea dhidi ya Pirates

Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kupata nguvu mpya katika safu yake ya ulinzi kuelekea mchezo dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, kufuatia kurejea kikosini kwa beki wake tegemeo, Ismail Toure.

Wekundu wa Msimbazi watashuka kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumapili, Novemba 29, kuikabili Orlando Pirates katika mchezo wa kwanza wa Kundi C wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Habari njema kwa mashabiki wa Simba ni kwamba huenda wakamshuhudia Toure akirejea uwanjani baada ya kukosa michezo mitatu iliyopita kutokana na majeraha.

Beki huyo amekuwa nje kwa wiki kadhaa akiuguza jeraha la goti, lakini alirejea kikosini mwanzoni mwa wiki hii kuelekea pambano hilo muhimu dhidi ya wababe hao wa Afrika Kusini.

Kurejea kwa Toure ni habari njema kwa kocha Steve Barker, kutokana na umuhimu wa beki huyo katika mfumo wa ulinzi wa Simba.

Tangu kujiunga kwake na Wekundu wa Msimbazi, Toure amekuwa nguzo muhimu katika safu ya ulinzi, akitengeneza pacha imara na beki wa kimataifa wa Afrika Kusini, Rushine de Reuck.

Iwapo Toure atakuwa fiti kucheza Jumapili, wawili hao watakuwa na jukumu kubwa la kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Orlando Pirates, wakishirikiana na wenzao katika eneo la ulinzi kuhakikisha lango la Simba linabaki salama.

Uimara wa safu hiyo utakuwa moja ya silaha muhimu kwa Simba katika harakati zake za kusaka alama tatu za kwanza kwenye hatua ya makundi.

Simba inahitaji kuanza vyema hatua hiyo, hasa kutokana na dhamira yake ya kufika nusu fainali ya michuano hiyo msimu huu, huku ikilenga kuvuna alama zote tisa katika michezo yake ya nyumbani.

Simba SC Stories

Semaji awatisha Orlando Pirates 'watake, wasitake watapasuka'
Semaji awatisha Orlando Pirates 'watake, wasitake watapasuka'
22m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Dozi ya Orlando Pirates inaandaliwa
Dozi ya Orlando Pirates inaandaliwa
14h ago
READ MORE →
Simba yazindua hamasa kuikabili Orlando Pirates, kaulimbiu ‘Huyu ni Wetu’
Simba yazindua hamasa kuikabili Orlando Pirates, kaulimbiu ‘Huyu ni Wetu’
20h ago
READ MORE →
Pirates wawasili Dar
Pirates wawasili Dar
23h ago
READ MORE →
Simba kuzindua hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Orlando Pirates leo
Simba kuzindua hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Orlando Pirates leo
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Kuzishuhudia Simba vs Orlando Pirates kiingilio buku saba
Kuzishuhudia Simba vs Orlando Pirates kiingilio buku saba
1d ago
READ MORE →
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
1d ago
READ MORE →
Pirates waanza safari kuifuata Simba
Pirates waanza safari kuifuata Simba
1d ago
READ MORE →