Semaji awatisha Orlando Pirates 'watake, wasitake watapasuka'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
32m ago
Semaji awatisha Orlando Pirates 'watake, wasitake watapasuka'

Kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, ametuma salamu za onyo kwa miamba ya soka kutoka Afrika Kusini, Orlando Pirates, akisisitiza kuwa watake wasitake watacha alama tatu jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa unatarajiwa kupigwa Jumapili hii, Novemba 29, 2026, katika Uwanja wa Uhuru, ambao kwa sasa unatumiwa na Simba kama ngome yao ya nyumbani kwa mashindano hayo ya kimataifa.

Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni maalum ya hamasa katika Tawi la Simba la Jangwani Mafuso eneo lililo karibu na makao makuu ya watani zao Yanga, Ahmed alisema Orlando Pirates wanaweza kuwa na historia kubwa, lakini watakutana na moto wa "Mnyama" katika uwanja huo ambao ameufananisha na tanuri la moto.

“Orlando apende, asipende atapasuka hapa Dar es Salaam. Watake wasitake lazima waache alama tatu kwenye Uwanja wa Uhuru. Lengo letu ni kuhakikisha alama zote tisa za mechi za nyumbani hazitoki nje ya nchi,” alisema Ahmed kwa kujiamini huku akishangiliwa na mashabiki.

Ahmed aliongeza kuwa kubadilishwa kwa uwanja kutoka Benjamin Mkapa na kwenda Uwanja wa Uhuru hakupunguzi makali ya klabu hiyo, bali kunawapa fursa ya kuweka rekodi mpya ya kimataifa katika uwanja huo mkongwe.

Ahmed ametoa wito kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili ili kuwajaza hofu wapinzani wao tangu dakika ya kwanza.

Amesisitiza kuwa ushindi hautapatikana kwa maneno ya majukwaani pekee, bali kwa hamasa na kelele za uwanjani zitakazowapa nguvu wachezaji.

Simba SC Stories

Toure tayari kurejea dhidi ya Pirates
Toure tayari kurejea dhidi ya Pirates
23m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
4h ago
READ MORE →
Dozi ya Orlando Pirates inaandaliwa
Dozi ya Orlando Pirates inaandaliwa
15h ago
READ MORE →
Simba yazindua hamasa kuikabili Orlando Pirates, kaulimbiu ‘Huyu ni Wetu’
Simba yazindua hamasa kuikabili Orlando Pirates, kaulimbiu ‘Huyu ni Wetu’
20h ago
READ MORE →
Pirates wawasili Dar
Pirates wawasili Dar
23h ago
READ MORE →
Simba kuzindua hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Orlando Pirates leo
Simba kuzindua hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Orlando Pirates leo
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Kuzishuhudia Simba vs Orlando Pirates kiingilio buku saba
Kuzishuhudia Simba vs Orlando Pirates kiingilio buku saba
1d ago
READ MORE →
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
1d ago
READ MORE →
Pirates waanza safari kuifuata Simba
Pirates waanza safari kuifuata Simba
2d ago
READ MORE →