Kuzishuhudia Simba vs Orlando Pirates kiingilio buku saba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22m ago
Kuzishuhudia Simba vs Orlando Pirates kiingilio buku saba

Klabu ya Simba SC imeanika rasmi viingilio vya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, mtanange unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka nchini.

Mchezo huo wa kukata na shoka unatarajiwa kupigwa Jumapili hii, Novemba 29, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.

Kupitia taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, uongozi wa Simba SC umeweka wazi viwango vya bei za tiketi, ambapo mashabiki wa kawaida watashuhudia burudani hiyo kwa kiasi cha chini cha Shilingi 7,000 tu (Buku Saba).

Mbali na jukwaa la Mzunguko, mashabiki wanaotafuta faraja zaidi watatakiwa kulipia Shilingi 40,000 kwa ajili ya jukwaa la VIP.

Kwa upande wa mashabiki wa hadhi ya juu wanaotaka kushuhudia mechi hiyo kwa mtindo wa kipekee, watakaa jukwaa la Platinum ambalo tiketi yake imewekwa kwa Shilingi 200,000.

Klabu ya Simba imesisitiza kuwa hakutakuwa na uuzaji wa tiketi za karatasi milangoni siku ya mchezo. Tiketi zote zinapatikana kwa njia ya kielektroniki kupitia tovuti rasmi ya SimbaSc.Wanaut.com

Simba SC Stories

Deen amerejea kuendeleza alipoishia
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
2h ago
READ MORE β†’
Pirates waanza safari kuifuata Simba
Pirates waanza safari kuifuata Simba
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 25 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 25 2026
6h ago
READ MORE β†’
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
20h ago
READ MORE β†’
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake
1d ago
READ MORE β†’
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
1d ago
READ MORE β†’