Klabu ya Simba imemrejesha mtaalamu wa uchambuzi wa mechi kutoka Afrika Kusini, Prinil Deen, kuimarisha benchi lake la ufundi.
Deen alijiunga kwa mara ya kwanza na Simba mwishoni mwa Desemba 2025, akiwa sehemu ya benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Steve Barker, kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu wa 2025/26.
Mtaalamu huyo alihudumu kwa takribani miezi saba ndani ya klabu hiyo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Tshepo Boshielo, ambaye pia ni raia wa Afrika Kusini.
Katika kurejea kwake, Deen atakuwa na jukumu la kuchambua video za mechi za Simba na wapinzani wake, kutathmini viwango vya wachezaji pamoja na kuandaa ripoti za kiufundi kwa ajili ya makocha.
Pia atahusika katika kulisaidia benchi la ufundi kupanga mbinu za mchezo kwa kuzingatia uwezo na udhaifu wa wapinzani.
Deen ana uzoefu wa kufanya kazi katika soka la Afrika Kusini, ambako amewahi kuhudumu katika klabu za Mamelodi Sundowns na Chippa United.
Kurejea kwa mtaalamu huyo kunatarajiwa kuimarisha maandalizi ya kiufundi ya Wekundu wa Msimbazi hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.