Pirates waanza safari kuifuata Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
50m ago
Pirates waanza safari kuifuata Simba

Miamba ya soka ya Afrika Kusini, Orlando Pirates, rasmi imeanza safari ya kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya mtanange mkali wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya wenyeji wao, Simba SC, mchezo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.

Pirates, wanaonolewa na kocha Jose Riveiro, wanaondoka nchini mwao wakiwa na morali ya juu baada ya ushindi thabiti wa mabao 2-0 walioupata Jumanne usiku dhidi ya Golden Arrows katika mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini (Betway Premiership).

Wakati Orlando Pirates wakitua nchini, wanakutana na Simba SC iliyo kwenye fomu ya hatari msimu huu. Chini ya kocha mkuu Steve Barker, Simba inaongoza Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania ikiwa na rekodi ya kipekee ya kushinda mechi zote 11 za kwanza za msimu, ikiwemo ushindi wa hivi karibuni wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Barker amewataka wachezaji wake kutobweteka na rekodi ya ligi ya ndani, akisisitiza kuwa michuano ya kimataifa inahitaji umakini wa hali ya juu, hasa dhidi ya timu kubwa kama Orlando Pirates.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kisasi na wenye ushindani mkubwa, ukirejesha kumbukumbu za mwaka 2022 ambapo timu hizi mbili zilikutana katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).

Katika michuano hiyo, Orlando Pirates ilifanikiwa kusonga mbele kwa mikwaju ya penalti baada ya jumla ya matokeo ya sare ya 1-1.

Pambano hilo linatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili, Novemba 29, 2026, kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemteua mwamuzi Abdel Aziz Bouh kutoka Mauritania kuamua sheria za mchezo huo, huku teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi (VAR) ikisimamiwa na Babacar Sarr.

Simba SC Stories

Deen amerejea kuendeleza alipoishia
Deen amerejea kuendeleza alipoishia
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 25 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 25 2026
4h ago
READ MORE β†’
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa
Simba yaomba kuongezwa mashabiki Ligi ya Mabingwa
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
Hii hapa siri ya Simba kushinda mechi mfululizo
18h ago
READ MORE β†’
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake
Libasse amtetea Doumbia, presha ni kubwa dhidi yake
1d ago
READ MORE β†’
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
1d ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
1d ago
READ MORE β†’