Nduda apania kurejesha makali yake

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
14 Sep 2018
Nduda apania kurejesha makali yake
Kipa Said Mohammed ‘Nduda’ ameanza upya katika kikosi cha Simba, baada ya kuonekana kubadili kabisa staili ya nywele zake kwa kutoa kiduku kichwani na kuongeza umakini kila zoezi lililokuwa linatolewa na kocha wake wa makipa Mohammed Mwalami.

Nduda aliyesimamishwa katika kikosi hicho hali na hakutambulishwa katika Tamasha la Simba Day amerejeshwa kikosini baada ya pande zote mbili kukaa chini na kuelewana.

Nduda alisema baada ya kukaa nje kwa muda mrefu amejifunza vitu vingi vya nje na ndani ya mpira, hivyo kurejea kwake katika kikosi anataka kuwa bora zaidi.

“Hahahaha nimeamua kuzipunguza tu, kweli nilikuwa nje lakini nilikuwa najifua kama kawaida na nimerudi kazini kikubwa kilichobaki ni kuipambania timu yangu ilifanya vizuri.”

Akizungumzia changamoto ya namba kutokana na makipa waliopo, Aishi Manula, Ally Salum na Deogratius Munishi kuonekana kuingia katika mifumo ya kocha Mbelgiji, Patrick Aussems, alisema suala hilo anamuachia mwalimu katika kupanga, lakini kikubwa wote ni wachezaji wazuri kikubwa matokeo yapatikane mazuri.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →