Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
42m ago
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa

Msisimko wa uchaguzi wa Klabu ya Simba SC unatarajiwa kuongezeka wiki hii, wakati Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikijiandaa kuweka hadharani majina ya wanachama watakaoruhusiwa kuendelea na kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa klabu hiyo.

Baada ya wanachama 48 kujitokeza kuchukua na kurejesha fomu, sasa jukumu limebaki mikononi mwa Kamati ya Uchaguzi kujiridhisha iwapo kila mmoja anastahili kuwania nafasi aliyoiomba.

Kamati hiyo itatumia siku za Jumatano na Alhamisi, Novemba 25 na 26, 2026, kupitia nyaraka za wagombea na kujiridhisha kuhusu utimilifu wa masharti yaliyowekwa katika Ibara ya 27(2) ya Katiba ya Simba.

Hivyo, Ijumaa ya Novemba 27 itakuwa siku muhimu kwa Wanasimba, kwani ndipo itakapofahamika iwapo majina yote yaliyotangazwa awali yataendelea kuwepo kwenye kinyang’anyiro au baadhi yataondolewa kutokana na kutokidhi vigezo.

Nafasi ya Mwenyekiti ndiyo inayovuta zaidi hisia za mashabiki kutokana na kujitokeza kwa wanachama saba, wakiwemo Murtaza Mangungu, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Swedy Mkwabi.

Wengine wanaowania kiti hicho ni Anindumi Jonas Semu, Mohamed Khamis Soloka, Dkt. Seif Ramadhani Muba na Selemani Haroub Said.

Ushindani pia unaonekana katika nafasi za Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, ambako wanachama 41 wamewasilisha maombi yao, wakiwemo watu wenye historia mbalimbali ya kuitumikia klabu hiyo.

Ingawa baadhi ya waliojitokeza tayari wameeleza maono na sababu za kutaka kuingia kwenye uongozi wa Simba, hatua ya uhakiki ndiyo itakayowapa nafasi ya kusonga mbele katika safari hiyo.

Simba SC Stories

Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
15h ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
18h ago
READ MORE β†’
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka
19h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
1d ago
READ MORE β†’
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
1d ago
READ MORE β†’
Tuna uwezo wa kushinda katika mazingira tofauti - Barker
Tuna uwezo wa kushinda katika mazingira tofauti - Barker
2d ago
READ MORE β†’
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
2d ago
READ MORE β†’