Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Simba kuweka hadharani viingilio vya mchezo dhidi ya Orlando Pirates Jumatano

Klabu ya Simba imepanga kutangaza rasmi viingilio vya mchezo wake dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema taarifa rasmi kuhusu viingilio pamoja na idadi ya mashabiki watakaoruhusiwa kuingia uwanjani zitatolewa kesho, Jumatano, Novemba 25, 2026.

“Taarifa kuhusu viingilio na idadi ya mashabiki kwa mchezo wetu dhidi ya Orlando tutatangaza rasmi Jumatano ya Novemba 25. Muhimu tuendelee kujiandaa nje na ndani ya uwanja kuelekea mchezo huo, lakini kubwa kabisa tuanze maandalizi ya kununua tiketi kwa wingi na kuhamasishana kwenye matawi, makundi na vijiwe vyetu,” alisema Ahmed Ally.

Kupitia kauli hiyo, uongozi wa Simba umewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuhamasishana ili kujitokeza kwa wingi kuipa nguvu timu yao katika mchezo huo muhimu wa kimataifa.

Simba itafungua pazia la hatua ya makundi kwa kuikaribisha Orlando Pirates Jumapili, Novemba 29, 2026, katika Uwanja wa Uhuru, maarufu kama Shamba la Bibi, jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi watakuwa na kibarua cha kusaka mwanzo mzuri katika hatua hiyo ya makundi, huku wakitarajia kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao watakapokuwa wakicheza nyumbani.

Simba kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliomba ongezeko la idadi ya mashabiki watakaoruhusiwa kuingia kwenye mchezo huo lengo likiwa kujaza uwanja wa Uhuru.

CAF iliiruhusu klabu ya Simba kuingiza mashabiki 6,000 tu kutokana na ukarabati wa miundombinu unaoendelea kwenye uwanja wa Uhuru.

Simba SC Stories

Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
Hatma ya wagombea wa nafasi za uongozi Simba kufahamika Ijumaa
42m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
Mawindo ya Orlando Pirates yameanza Mo Simba Arena
15h ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
Tuko tayari kukabiliana na yeyote CAFCL - Maema
18h ago
READ MORE β†’
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka
19h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
1d ago
READ MORE β†’
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
1d ago
READ MORE β†’
Tuna uwezo wa kushinda katika mazingira tofauti - Barker
Tuna uwezo wa kushinda katika mazingira tofauti - Barker
2d ago
READ MORE β†’
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
2d ago
READ MORE β†’