Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11m ago
Barker kuongea dozi Simba kukabiliana na ushindani unoongezeka

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amekiri kuwa kazi ya kuendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100 kwenye Ligi Kuu ya NBC inazidi kuwa ngumu, huku akipanga kuongeza dozi ya maandalizi na mbinu ili kuhakikisha Wekundu wa Msimbazi wanaendelea kuwapa wakati mgumu wapinzani wao.

Simba imekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu, ikikusanya pointi zote 33 katika michezo 11 iliyocheza, bila kupoteza mchezo wala kutoka sare. Hata hivyo, rekodi hiyo imeanza kugeuka kuwa mtihani mkubwa kwa Barker, kwani kila timu inayokutana na Simba inaingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kuwa ya kwanza kusimamisha kasi yao.

Barker amebainisha kuwa kadiri msimu unavyosonga mbele, ndivyo wapinzani wanavyozidi kujiandaa kwa nguvu zaidi, hali inayomlazimu kuendelea kutafuta mbinu mpya za kuhakikisha kikosi chake kinabaki kwenye njia ya ushindi.

"Ukiangalia katika mechi chache zilizopita unaweza kuona vile kumekuwa na changamoto kwa sababu kila timu ina lengo lake na inataka kuvunja mfululizo wetu wa ushindi. Tunachopaswa kufanya sisi kama timu ni kuendelea kuonyesha mentaliti imara na tabia ya kushinda," amesema Barker.

USHINDI WA JKT WAMPA BARKER SOMO!

Kauli hiyo imekuja baada ya Simba kulazimika kupambana kwa nguvu kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania, mchezo ambao Wekundu wa Msimbazi walijikuta wakitanguliwa kabla ya kupindua matokeo.

Kwa Barker, ushindi huo haukuwa tu wa kuongeza pointi tatu, bali pia ulithibitisha namna ambavyo wachezaji wake wamejenga tabia ya kupambana hadi mwisho bila kukata tamaa.

Kocha huyo amesisitiza kuwa Simba inapaswa kuwa tayari kushinda katika mazingira yoyote, iwe kwa mabao mengi au kwa kupambana hadi dakika za mwisho, kwani kila mchezo una changamoto zake.

Uwezo huo umeonekana pia katika michezo mingine migumu, ikiwemo Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga ambayo Simba ilishinda mabao 2-1, pamoja na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo baada ya kutoka nyuma.

Matokeo hayo yameendelea kuimarisha imani ya Barker kwa wachezaji wake, ambao wameonyesha uwezo wa kubadili matokeo hata wanapokuwa katika mazingira magumu.

ORLANDO PIRATES SASA KIPIMO KINGINE!

Wakati Simba ikiendelea kulinda rekodi yake ya kutopoteza mchezo kwenye ligi, macho sasa yanaelekezwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako inatarajiwa kukutana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Simba inatarajiwa kuingia kambini leo Jumatatu, Novemba 23, kuanza maandalizi ya mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi utakaochezwa Jumapili, Novemba 29, 2026, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Huu utakuwa mtihani mwingine wa kuthibitisha uimara wa kikosi cha Simba, hasa ikizingatiwa kuwa ushindani wa kimataifa unahitaji umakini mkubwa, nidhamu ya hali ya juu na matumizi sahihi ya nafasi.

Simba SC Stories

Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
Huyu Libasse Gueye ni namba ya kutisha!
5h ago
READ MORE β†’
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
Simba vs Orlando Pirates ni Jumapili CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
8h ago
READ MORE β†’
Tuna uwezo wa kushinda katika mazingira tofauti - Barker
Tuna uwezo wa kushinda katika mazingira tofauti - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
Highlights : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL, Nov 21
FT : JKT Tanzania 1-2 Simba, NBC PL, Nov 21
1d ago
READ MORE β†’
Orodha ya wagombea waliochukua fomu Simba
Orodha ya wagombea waliochukua fomu Simba
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Simba, NBC PL, Nov 21
Kikosi : JKT Tanzania vs Simba, NBC PL, Nov 21
1d ago
READ MORE β†’
Simba ugenini dhidi ya JKT Tanzania leo, NBC PL
Simba ugenini dhidi ya JKT Tanzania leo, NBC PL
2d ago
READ MORE β†’