Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa orodha ya wanachama 48 wa Simba SC waliochukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo, huku nafasi ya Mwenyekiti ikiwa na wagombea saba na nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ikiwa na wagombea 41.
Orodha hiyo imetolewa baada ya kukamilika kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu lililoanza Novemba 16 na kuhitimishwa Novemba 20, 2026, katika ofisi za TFF zilizopo Karume, jijini Dar es Salaam.
Katika nafasi ya Mwenyekiti, majina yaliyomo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Murtaza Ally Mangungu, aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Irick Nyange 'Kaburu', pamoja na Swedy Khamis Mkwabi.
Wengine waliochukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo ni Anindumi Jonas Semu, Mohamed Khamis Soloka, Dkt. Seif Ramadhani Muba na Selemani Haroub Said.
Kujitokeza kwa Mangungu kunamaliza sintofahamu iliyokuwepo kuhusu iwapo angewania tena nafasi hiyo, baada ya baadhi ya wanachama waliotangaza nia ya kugombea kueleza kuwa walikuwa wakisubiri kuona uamuzi wake.
Kwa upande wa nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, jumla ya wanachama 41 wamejitokeza, wakiwemo baadhi ya majina yanayofahamika kwa mashabiki wa Simba.
Miongoni mwao ni Hassan Bakari Kakayoo, maarufu kama Mzee wa Salute, mchezaji wa zamani wa Simba Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio', Christopher Kabalika Mwansasu, Wilfred Elias Nyamwija, Said Hassan Tully na Yusuph Omary Yenga.
ORODHA KAMILI YA WALIOCHUKUA NA KUREJESHA FOMU
Nafasi ya Mwenyekiti – Wagombea 7
-
Anindumi Jonas Semu
-
Geofrey Irick Nyange
-
Mohamed Khamis Soloka
-
Murtaza Ally Mangungu
-
Dkt. Seif Ramadhani Muba
-
Selemani Haroub Said
-
Swedy Khamis Mkwabi
Nafasi ya Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi – Wagombea 41
-
Aaron Henry Mrina
-
Abdallah Rashid Mgomba
-
Alfred Martin Elia
-
Andrew Julius Tupa
-
Arnold Nzuamtemi Nzali
-
Aziz Hussein Kaku
-
Christopher Kabalika Mwansasu
-
Damian Samweli Manembe
-
Eli Achahofu Paulo
-
Enock Bwigane Mwasubila
-
Fadhili Mohamed Famonga
-
Farid Awadh Tamim
-
Francis Kumba Ndulane
-
Hamisi Omari Tika
-
Hassan Bakari Kakayoo
-
Hussein Ally Simba
-
Isabella Samwel Faya
-
Issa Masoud
-
Jamhuri Mussa Kihwelo
-
Jonathan Wilisaa Nkya
-
Juma Abbas Pinto
-
Laurian Salvatory Mganga
-
Mariam Abdallahi Ibrahim
-
Mariam Mussa Shemzigwa
-
Muhamadi Mohamed Hamisi
-
Omari Juma Mazola
-
Pendo Aidan Mapugio
-
Rachel Juma Chagonja
-
Raphael Masunga Chegeni
-
Richard Shukia
-
Rodney Makamba Chiduo
-
Said Hassan Tully
-
Saidi Abdallah Njechele
-
Saleh Mohamed Afif
-
Salum Issaka Hamidu
-
Salum Kassim Maftah
-
Shukuru Athumani Mtego
-
Dkt. Suleiman Serera
-
Ussi Salum Pondeza
-
Wilfred Elias Nyamwija
-
Yusuph Omary Yenga
Orodha iliyotolewa na TFF ni ya waliochukua na kurejesha fomu, hivyo haimaanishi kuwa wote tayari wamepitishwa rasmi kuwa wagombea wa mwisho.
Hatua zinazofuata za mchakato wa uchaguzi, ikiwemo uhakiki wa sifa, mapingamizi na taratibu nyingine, ndizo zitakazosaidia kubainisha watakaoruhusiwa kuendelea na kinyang'anyiro hicho.