Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inarejea leo baada ya mapumziko ya takribani wiki tatu kupisha kalenda ya FIFA.
Mechi tatu zinatarajiwa kupigwa leo huku vinara wa ligi hiyo Simba wakitarajiwa kushuka dimbani kesho Jumamosi.
Simba itachuana na JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Isamuhyo saa 12:30 jioni.
Unaweza kusema baada ya mashabiki wa Simba kuikosa burudani kutoka kwa timu yao kwa wiki tatu, hatimaye raha zimerejea!
