Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1d ago
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker

Kurejea kwa mabeki Shomary Kapombe, Wilson Nangu, Abdurlazack Hamza na Vedastus Masinde baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha, kumemuongezea mzuka Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker.

Mabeki hao wameanza kurejea taratibu uwanjani, ikiwa ni habari njema kwa Wekundu wa Msimbazi ambao wanaendelea kufanya vizuri katika mashindano ya ndani huku wakijiandaa na changamoto za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Barker ameanza kuwapa dakika za kucheza wachezaji hao kupitia michezo ya kirafiki, lengo likiwa ni kuwajengea utimamu wa mwili kabla ya kuwatumia katika michezo ya ushindani.

Katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya Mashujaa FC, wachezaji wote walipata nafasi ya kucheza.

Barker ameeleza kufurahishwa na urejeo wa wachezaji hao huku akiweka wazi kuwa hana haraka ya kuwatumia wachezaji hao katika michezo ya ushindani, badala yake anataka kuwajenga hatua kwa hatua kulingana na hali zao za utimamu wa mwili.

Kurejea kwa Kapombe katika eneo la beki wa kulia, pamoja na Nangu, Hamza na Masinde katika eneo la ulinzi wa kati, kutamuongezea Barker wigo mpana wa uchaguzi wa wachezaji katika kikosi chake.

Aidha wakati huu ambo Simba imepata pigo baada ya mlinzi wa kulia Nathaniel Chilambo kuumia wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa, urejeo wa Kapombe ni habari njema kwani ataweza kushirikiana na David Kameta kuhakikisha pengo la Chilambo linazibwa.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 19 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Novemba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’