Vita ya kuwania ufalme wa mabao ndani ya kikosi cha Simba SC katika Ligi Kuu ya NBC imezidi kupamba moto, huku Elie Mpanzu, Clatous Chama na Anicet Oura wakiwa jino kwa jino katika mbio hizo.
Nyota hao watatu kila mmoja amefunga mabao manne, wakiongoza orodha ya wafungaji bora wa Wekundu wa Msimbazi katika ligi hiyo.

Mabeki Ismail Toure na Rushine de Reuck nao hawako nyuma katika vita hiyo, kila mmoja akiwa amefunga mabao matatu.
Mchango wa mabeki hao unaonyesha namna kikosi cha Simba kinavyopata mabao kutoka maeneo mbalimbali ya uwanja bila kutegemea washambuliaji pekee.
Libasse Gueye anafuatia akiwa amezifumania nyavu mara mbili, huku Neo Maema na Morice Abraham kila mmoja akiwa na bao moja.
Katika jumla ya mabao 23 yaliyofungwa na wachezaji hao wanane, Mpanzu, Chama na Oura wamechangia mabao 12, sawa na asilimia 54.5 ya mabao hayo.
Libasse ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi kwani licha kufunga mabao mawili, pia ametoa asiti saba.