Mzee wa Saluti ajitosa kuwania Ujumbe Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2d ago
Mzee wa Saluti ajitosa kuwania Ujumbe Simba

Mwanachama wa Klabu ya Simba SC, Hassan Bakari Kakayoo, maarufu kama Mzee wa Saluti, amejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza leo, Novemba 18, 2026, katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam, Kakayoo amesema uamuzi wake wa kuchukua fomu unatokana na kutekeleza haki yake ya msingi ya kikatiba kama mwanachama wa Simba.

Mzee wa Saluti amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwezesha kufika salama na kukamilisha hatua hiyo muhimu, huku akisisitiza kuwa bado kuna taratibu na miongozo inayopaswa kufuatwa kabla ya kuzungumzia kwa kina masuala ya kampeni.

Kakayoo amefichua kuwa hii ni mara yake ya pili kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo, baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2022, ambapo hadi sasa amehifadhi risiti pamoja na nyaraka za wakati huo kama vielelezo.

Akihitimisha mazungumzo yake, Mzee wa Saluti amesema amemkabidhi Mwenyezi Mungu safari yake ya kuwania nafasi hiyo.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’