Chilambo atakosekana kwa wiki tatu hadi nne

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2d ago
Chilambo atakosekana kwa wiki tatu hadi nne

Klabu ya Simba SC imepata pigo kuelekea kuanza kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya beki wake wa kulia, Nathaniel Chilambo, kupata majeraha akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Chilambo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu hadi nne kufuatia majeraha aliyoyapata jana, Novemba 17, 2026, katika mchezo dhidi ya Nigeria uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa vipimo vya kitabibu alivyofanyiwa baada ya mchezo huo vimebaini kuwa beki huyo amepata jeraha la kuchanika kwa kano (ligament), hali itakayomlazimu kuwa nje ya uwanja kwa kipindi hicho.

Chilambo alishindwa kuendelea na mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za AFCON 2027, akilazimika kutolewa dakika ya 29 na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul Sopu. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

PIGO KWA STEVE BARKER

Majeraha ya Chilambo yamekuja katika kipindi ambacho Simba inajiandaa na ratiba ngumu ya mashindano ya ndani pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Beki huyo, aliyesajiliwa kutoka Azam FC Julai mwaka huu, amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika kikosi cha Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, akifanya vizuri katika nafasi ya beki wa kulia wakati Shomari Kapombe akiwa nje kutokana na majeraha.

Kutokana na muda anaotarajiwa kukaa nje, Chilambo yupo katika hatari ya kukosa mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Orlando Pirates, pamoja na baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Bara.

KAPOMBE KUWA TEGEMEO

Licha ya pigo hilo, habari njema kwa Simba ni kurejea kwa beki mkongwe Shomari Kapombe, ambaye hivi karibuni alianza kupata dakika za kucheza baada ya kupona jeraha la bega alilolipata wakati wa michuano ya Kombe la Kagame nchini Rwanda.

Kapombe alipata nafasi ya kucheza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mashujaa, ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kurejea kwake kunaweza kumpa Barker suluhisho la muda katika upande wa kulia wa safu ya ulinzi wakati Chilambo akiendelea na matibabu.

CHILAMBO AAHIDI KUREJEA KWA NGUVU

Kupitia ujumbe wake baada ya kupata majeraha hayo, Chilambo amewashukuru Watanzania kwa upendo na sapoti waliyoonyesha kwake, akisisitiza kuwa kuvaa jezi ya Taifa Stars ni heshima kubwa katika maisha yake.

Beki huyo ameahidi kupambana ili kurejea uwanjani akiwa imara zaidi.

Iwapo matibabu yatakwenda kama inavyotarajiwa, Chilambo anaweza kurejea uwanjani katikati ya Desemba, ingawa muda halisi utategemea maendeleo ya matibabu yake.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’