Mwamuzi kutoka Mauritania, Abdel Aziz Bouh, ameteuliwa kuchezesha mchezo wa kwanza wa Kundi C hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kati ya Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini utakaopigwa Novemba 29, 2026.
Mchezo huo utakaofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam utakuwa mwanzo wa safari ya timu hizo katika harakati za kuwania nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Katika uteuzi huo, raia mwenzake wa Mauritania, Babacar Sarr, atakuwa mwamuzi wa teknolojia ya video (VAR), akisaidia usimamizi wa mchezo huo.
Simba itakuwa na jukumu la kutumia vyema faida ya kucheza nyumbani kwa kuanza kampeni yake ya hatua ya makundi kwa matokeo mazuri dhidi ya Orlando Pirates, timu yenye ushindani mkubwa kutoka Afrika Kusini.
Baada ya kutofanya vyema msimu uliopita, msimu huu Simba imepania kuvuka hatua ya robo fainali.