Wanachama zaidi wajitokeza kuchukua fomu kuwania uongozi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3d ago
Wanachama zaidi wajitokeza kuchukua fomu kuwania uongozi Simba

Mchakato wa uchaguzi wa viongozi wapya wa Klabu ya Simba umeendelea kushika kasi baada ya wanachama zaidi kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, huku ajenda za umoja, mabadiliko ya klabu na ushirikishwaji wa vijana zikitawala kwa baadhi ya wanaotaka kuingia madarakani.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wakili Kiomoni Kibamba, amesema zoezi la uchukuaji wa fomu linaendelea vizuri na kwa utaratibu uliopangwa.

Kibamba amesema hayo wakati akizungumzia mwenendo wa mchakato huo ambao TFF imeamua kuusimamia kufuatia kuwepo kwa mvutano kati ya pande mbili kuhusu usimamizi wa uchaguzi huo.

"Hadi sasa zoezi la kuchukua fomu linaendelea vizuri, kila kitu kinaenda sawa, hilo ndilo ninaloweza kuzungumza kwa sasa," amesema Kibamba.

Zoezi hilo lilianza rasmi Novemba 16, 2026, ambapo miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu ni Geofrey Nyange Kaburu anayewania nafasi ya mwenyekiti pamoja na Christopher Mwansasu anayewania nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Leo, Novemba 17, 2026, Agness Daniel maarufu kama 'Aggy Simba' naye amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe wa klabu hiyo.

Wengine waliojitokeza katika mchakato huo ni mwanachama Francis Kumba Ndulane, aliyechukua fomu ya kuwania ujumbe wa bodi ya klabu akieleza kuwa ana uzoefu wa kutosha katika shughuli za Simba na anaamini anaweza kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya timu hiyo.

Ndulane, ambaye ni mwanachama hai wa tawi la Ifakara na amewahi kuwa kiongozi wa tawi hilo, amesema uzoefu wake unahusisha pia kushiriki misafara ya timu, ikiwamo safari ya Zambia Desemba 2018 kwa ajili ya mchezo dhidi ya Nkana, akiwa kiongozi wa msafara.

Kwa upande mwingine, Anindumi Jonas ametangaza nia ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Simba, akibeba ajenda kuu tatu ambazo ni mabadiliko ya klabu, kuboresha mfumo wa uanachama na kuwapa vijana nafasi katika uongozi.

Jonas amesema amekuwa mwanachama wa Simba kwa miaka 20, amesisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu unaoeleweka katika mchakato wa mabadiliko ya klabu hiyo ili kuhakikisha uendeshaji wake unakuwa katika mfumo mzuri na wenye mwelekeo.

Naye Christopher Kabalika Mwataso amejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Mjumbe baada ya kufika katika ofisi za TFF Novemba 16, 2026.

Mwataso amesema dhamira yake ni kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ili kupata nafasi ya kuwatumikia wanachama na kusaidia kuiongoza Simba katika hatua bora zaidi, akiahidi kueleza kwa kina mipango na matarajio yake baada ya kukamilika kwa zoezi la uchukuaji wa fomu.

Farid Awadhi nae ametangaza nia ya kuwania nafasi ya ujumbe wa klabu hiyo, akieleza kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kuunganisha wanachama na kuondoa makundi yanayoonekana kujitokeza ndani ya Simba.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Kibamba, uchaguzi huo utafanyika Januari 30, 2027, badala ya Januari 3 kama ilivyokuwa imepangwa awali. Hatua hiyo inalenga kuwawezesha viongozi watakaochaguliwa kupokea rasmi majukumu kutoka kwa viongozi wanaomaliza muda wao chini ya mwenyekiti wa sasa, Murtaza Ally Mangungu.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’