Mashabiki, Wanachama Simba watinga TFF, wafikisha malalamiko

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
3d ago
Mashabiki, Wanachama Simba watinga TFF, wafikisha malalamiko

Mamia ya wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba SC, leo Jumanne, Novemba 17, 2026, wamefanya maandamano ya amani hadi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizopo Karume, Dar es Salaam, kupinga mchakato na usimamizi wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliotangazwa na shirikisho hilo.

Maandamano hayo yanakuja kufuatia kutoridhishwa na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo kuwa Januari 30, 2027, huku mashabiki na uongozi wa Simba wakisisitiza uchaguzi huo unapaswa kufanyika mapema zaidi, mnamo Januari 3, 2027.

Wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, mashabiki hao walisikika wakipaza sauti kupinga Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuingilia na kusimamia uchaguzi wao. Baadhi ya ujumbe kwenye mabango hayo ulisomeka: “Hatutaki TFF isimamie uchaguzi wetu,” “Tunapenda amani lakini tunataka haki,” na “Mangungu Must Go,” wakishinikiza pia kuondoka kwa Mwenyekiti wa sasa wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu.

Sintofahamu imekuwa kubwa baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC kuonyesha kutoridhishwa na kitendo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mustakabali wa uchaguzi wa klabu hiyo, badala ya kujibu barua rasmi waliyoituma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba iliyotolewa hivi karibuni, klabu hiyo iliwasilisha barua TFF mnamo Novemba 13, 2026, ikieleza msimamo na mapendekezo yao ya kisheria kuelekea uchaguzi huo, na walitegemea kupata majibu rasmi kwa njia ya kimaandishi kuliko kusikia majibu hayo yakitolewa kwenye vyombo vya habari.

Simba imesisitiza kuwa klabu ipo salama na inaongozwa kwa misingi ya katiba yao, huku wakitaka taratibu zote za uchaguzi zifuate matakwa ya wanachama na si shinikizo la nje. 

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE →
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE →
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE →
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE →
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE →
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE →
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE →
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE →
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE →