Mbio za kuwania kiti cha Uenyekiti wa Klabu ya Simba zimepamba moto kufuatia aliyekuwa Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, kuchukua rasmi fomu ya kuwania nafasi hiyo ya juu, huku aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), Barbara Gonzalez, akipigiwa chapuo kubwa na wanachama.
Mchakato huo wa kuchukua fomu ulioanza leo, umeweka wazi kuwa uchaguzi mkuu ujao wa klabu hiyo utakuwa mmoja wa chaguzi zenye ushindani mkubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uzito wa majina ya makada wanaotajwa na waliojitokeza.
Kaburu, ambaye ana uzoefu wa muda mrefu katika uongozi ndani ya klabu ya Simba, anafahamika kwa ushawishi wake mkubwa miongoni mwa wanachama wa zamani na wapya.
Wakati Kaburu akichukua fomu, kundi kubwa la wanachama na mashabiki wa klabu hiyo limeonekana kuelekeza nguvu zake kwa Barbara Gonzalez.
Mtendaji huyo wa zamani anapigiwa chapuo kubwa kutokana na rekodi yake ya utendaji wa kisasa, uwezo wa kusimamia mifumo ya kifedha ya klabu, na uhusiano wake mzuri na wawekezaji pamoja na mashabiki.
"Simba inahitaji kiongozi anayejua soka la kisasa na biashara, na Barbara amethibitisha hilo wakati akiwa CEO. Tunamwomba aingie kwenye mchuano huu," alisema mmoja wa wanachama wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi wa klabu ya Simba umepangwa kufanyika Januari 30 2027 mchakato kuelekea uchaguzi huo ukianza rasmi leo