Simba yakosa imani na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi TFF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4d ago
Simba yakosa imani na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi TFF

Klabu ya Simba SC imeibua maswali mazito kuhusu mwenendo wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ikieleza kutoridhishwa na namna ambavyo amekuwa akishughulikia masuala yanayohusu klabu hiyo, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Novemba 15, 2026, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imeweka wazi msimamo wake kuhusu mwenendo wa mchakato wa uchaguzi, huku ikieleza kutoridhishwa na kitendo cha Mwenyekiti huyo kujibu barua rasmi ya klabu kupitia vyombo vya habari badala ya kutumia utaratibu rasmi wa mawasiliano.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Simba iliiandikia TFF barua rasmi Novemba 13, 2026, ikiwasilisha msimamo wake kuhusu mwenendo wa mchakato wa uchaguzi, kutoa mapendekezo ya maboresho na kuomba majibu rasmi kwa maandishi.

Hata hivyo, klabu hiyo imesema haioni kuwa ni sahihi kwa kiongozi wa chombo kinachosimamia uchaguzi wa mpira wa miguu kujibu barua rasmi ya klabu kupitia vyombo vya habari kabla ya kuipatia klabu majibu ya maandishi.

Simba imeomba TFF kutoa majibu rasmi ya maandishi kupitia barua hiyo.

Katika hatua nyingine, Simba imepinga kauli iliyotolewa na Mwenyekiti huyo kuhusu uwepo wa pande mbili zinazopingana ndani ya klabu.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa kuna ofisi mbili, moja ya Mwekezaji iliyopo Masaki na nyingine ya Mwenyekiti Murtaza Mangungu iliyopo Msimbazi.

Simba imeeleza kuwa kauli hiyo si sahihi kwa kuwa inatoa taswira ya kuwepo kwa taasisi mbili tofauti ndani ya klabu moja.

Bodi hiyo imesema kauli hizo zinaweza kuongeza mkanganyiko miongoni mwa wanachama na wadau wa klabu, huku zikiwa na athari za kisheria.

Msisitizo wa Simba ni kwamba ni taasisi moja na inapaswa kutambuliwa hivyo na kila mdau anayehusika na masuala ya uchaguzi.

SIMBA YATAKA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI

Pamoja na hoja hizo, Bodi ya Wakurugenzi imesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha uchaguzi wa klabu unakuwa huru, wa haki, wazi na unaoaminika.

Simba imeeleza kuwa msimamo wake unatokana na Katiba ya klabu, Kanuni zake za Uchaguzi pamoja na kanuni za TFF na FIFA, katika misingi ya kuheshimiana na kuelewana.

Aidha, klabu imesema hatua zaidi za kisheria zitazingatiwa dhidi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’