Katika maandalizi ya kikosi cha Simba wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA, leo kumepigwa mchezo wa kirafiki kati ya Wekundu wa Msimbazi dhidi ya Mashujaa Fc.
Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa kambani na mshambuliaji Elie Mpanzu.
Mchezo huo ni sehemu ya mechi za kirafiki ambazo kocha Steve Barker amezihitaji katika kukiimarisha kikosi chakee.







