Simba yatajwa kumnyemelea mshambuliaji Mnigeria, Ighodaro

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Nov 2026
Simba yatajwa kumnyemelea mshambuliaji Mnigeria, Ighodaro

Kuelekea usajili wa dirisha dogo, jina la mshambuliaji wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Etiosa Ighodaro, likitajwa kwenye rada za vinara wa ligi kuu ya NBC, Simba SC.

Inaelezwa kuwa wekundu wa Msimbazi wameanza kufanya tathmini ya uwezekano wa kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji, na jina la Ighodaro limeingia kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kuwindwa.

Mshambuliaji huyo mwenye uraia wa Nigeria anatajwa kuwa miongoni mwa chaguo zinazovutia kutokana na uzoefu wake katika soka la Afrika Kusini, ambako amewahi kuzitumikia klabu mbalimbali ikiwemo Chippa United, SuperSport United na AmaZulu kabla ya kujiunga na Kaizer Chiefs.

Simba imetajwa kuwa na nia ya kufanya jaribio la kumpata nyota huyo, ikiamini anaweza kuongeza makali katika eneo la ushambuliaji.

Kinachoongeza nguvu kwenye tetesi hizi ni madai kwamba mshambuliaji huyo anataka kuondoka Chiefs baada ya kutohakikiwa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs.

Cheifs wanaweza kuridhia hata kumtoa kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili la Januari 2027. Hiyo inaweza kuwa fursa kwa Simba kujaribu kumshawishi kuhamia Tanzania.

Simba imeanza mapema msako wa mshambuliaji anayeweza kuwa mbadala wa Ibrahim Doumbia ambaye bado hajaweza kuonyesha ushawishi wa kulinda nafasi yake.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’