Kiungo mshambuliaji wa Simba Bakari Msimu amerejea nchini baada ya kukamilisha majaribo nchini Austria.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 18, amerea Simba baada ya kumaliza majaribio ya Siku tano na klabu ya Austria,SKN St. Polten.
Wakati akisubiri hatma ya majaribio hayo amerejea kuendelea na majukumu yake katika kikosi cha Simba.
Uongozi wa Simba umewazi msimamo wake kuwa mchezaji huyo ruksa kujiunga na miamba hao kama atafuzu majaribio yake