Nangu, Abdulrazack Hamza wakaribia kurejea kikosini, kuongeza ushindani safu ya ulinzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Nov 2026
Nangu, Abdulrazack Hamza wakaribia kurejea kikosini, kuongeza ushindani safu ya ulinzi

Habari njema kwa mashabiki wa Simba SC ni kwamba safu ya ulinzi ya timu hiyo inatarajiwa kupata nguvu zaidi kufuatia mabeki wa kati Wilson Nangu na Abdulrazack Hamza kukaribia kurejea uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

Mabeki hao wawili wameanza kuonyesha dalili nzuri za kuimarika baada ya kuanza programu maalumu za mazoezi mepesi pamoja na mazoezi ya kurejesha utimamu wa mwili (fitness), hatua inayowapa matumaini mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kuwa hivi karibuni wataungana tena na wenzao katika kikosi cha kwanza.

Wilson Nangu alilazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kifundo cha mguu nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu, hali iliyomfanya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Hata hivyo, beki huyo ameendelea kuimarika na kwa sasa anaonyesha maendeleo mazuri katika programu yake ya kurejea dimbani. 

Kwa upande mwingine, Abdulrazack Hamza naye anaendelea na mazoezi maalumu ya viungo kwa lengo la kurejesha nguvu na utimamu wa mwili baada ya kukabiliwa na majeraha yaliyomweka nje kwa miezi kadhaa.

Iwapo mabeki hao watarejea kikamilifu, Simba SC itakuwa na machaguo zaidi katika eneo la ulinzi, jambo litakaloongeza ushindani wa kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Kwa sasa, safu hiyo inaongozwa na mabeki wenye uzoefu Rushine de Reuck na Ismail Toure ambaye hata hivyo aliapata majeraha ambayo yatamlazimu kukaa nje kwa takribani wiki tatu.

Licha ya maendeleo mazuri yanayoonekana, madaktari wa klabu hiyo wanaendelea kuwasimamia kwa karibu wachezaji hao ili kuhakikisha wanarejea wakiwa wamepona kikamilifu.

Wachezaji hao wamekaa nje kwa muda mrefu kutokana na aina ya kajeraha waliyopata uongozi wa Simba ukihakikisha wanapona kikamilifu kabla ya kurejea tena uwanjani.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’