Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake Mo Simba Arena kujiandaa na mechi zinazofuata za ligi kuu na ligi ya mabingwa hatua ya makundi.
Baada ya mpango wa kusafiri nchini Kenya kukwama, kikosi cha Simba kesho Jumamosi kinatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mashujaa Fc.
Mchezo huo ni sehemu ya mpango mkakati wa benchi la ufundi katika kuhakikisha wachezaji wanarejesha utimamu wao wa kimchezo baada ya mapumziko.
Mchezo huo ni wa ndani na hautahudhuriwa na mashabiki.