Hofu ya Ebola yakwamisha mipango ya Simba kuweka kambi Kenya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Nov 2026
Hofu ya Ebola yakwamisha mipango ya Simba kuweka kambi Kenya

Klabu ya Simba SC imelazimika kutafakari upya mpango wake wa kuweka kambi ya maandalizi nchini Kenya, kufuatia hofu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na masharti ya usafiri yanayoweza kuathiri safari yake ya kuelekea Morocco.

Simba ilikuwa imepanga kutumia muda nchini Kenya kujiandaa kwa michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara. Hata hivyo, hali ya kiafya inayohusishwa na Ebola imeibua wasiwasi ndani ya klabu hiyo na kufanya mpango huo kuwa na mashaka.

Mbali na suala la usalama wa kiafya, kuna kikwazo kingine kinachohusiana na taratibu za kuingia nchini Morocco. Masharti yaliyowekwa na nchi hiyo yanawataka wasafiri wanaotoka Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) na Uganda kusubiri siku 30 tangu walipotoka katika mataifa hayo kabla ya kuruhusiwa kuingia Morocco.

Hali hiyo imeifanya Simba kuwa makini zaidi, kwani ina safari muhimu ya kucheza na RS Berkane nchini Morocco katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaofanyika kati ya Desemba 18 na 20, 2026.

Akizungumzia suala hilo, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, ameeleza kuwa uongozi bado unalifanyia tathmini kuhusu mkakati wao wa maandalizi. Amesema taarifa rasmi kuhusu uamuzi wa mwisho inatarajiwa kutolewa ndani ya siku mbili zijazo.

Awali, Wekundu wa Msimbazi walikuwa wamekubali mwaliko wa Gor Mahia ya Kenya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika Novemba 15, 2026. Mechi hiyo ni sehemu ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’