Barker aweka mkakati wa kuendeleza ubabe CAFCL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Nov 2026
Barker aweka mkakati wa kuendeleza ubabe CAFCL

Wakati kikosi chake kikirejea mazoezini baada ya mapumziko, Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amehitaji angalau mechi mbili za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.

Msimu huu Barker na vijana wake wameuanza kibabe wakishinda mechi zote walizocheza kwenye mashindano yote.

Mkakati wa Simba ni kuhakikisha wanaendeleza moto huo mkakati maalum ukiwekwa kwenye ligi ya mabingwa ambapo Wekundu wa Msimbazi wanahitaji kuvuka hatua ya makundi.

Barker ameeleza umuhimu wa mechi hizo za kirafiki akiamini zitasaidia katika kukiandaa kikosi chake kiushindani kuelekea kwenye ratiba hiyo inayofuata baada ya mapumziko ya FIFA.

“Tunafahamu kuwa hatua ya makundi ni ushindani tofauti na ule tuliokutana nao katika raundi za awali. Tunahitaji kutumia kipindi hiki kuboresha maeneo ambayo tuliona changamoto, kuongeza ushindani ndani ya kikosi na kuhakikisha wachezaji wanaingia katika michezo hiyo wakiwa tayari. Lengo letu ni kushindana na kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita.”

"Michezo ya kirafiki ni sehemu muhimu ya maandalizi kwa sababu inatupa nafasi ya kupima namna mbalimbali ya uchezaji, kuimarisha maelewano baina ya wachezaji na kutathmini utimamu wao kabla ya kukutana na wapinzani wenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya Afrika," alisema

Awali Simba ilialikwa nchini Kenya kushiriki kumbukumbu ya Raila Odinga, hata hivyo changamoto ya ugonjwa ebola huenda ikakwamisha mpango huo.

Simba SC Stories

Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
Wagombea zaidi wajitokeza siku ya mwisho kuchukua fomu Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
Barker apania kuendeleza wimbi la ushindi baada ya mapumziko ya FIFA
14h ago
READ MORE β†’
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
Miquissone aibukia Singida BS, arejea tena Ligi Kuu Tanzania
17h ago
READ MORE β†’
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
Zoezi la kuchukua fomu Simba kuhitimishwa leo
17h ago
READ MORE β†’
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
Ligi Kuu inarejea leo baada ya mapumziko ya FIFA, Mnyama dimbani Jumamosi
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
Mchungaji wa Simba achukua fomu Uenyekiti wa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
Simba kinara wa mabao ya mipira ya kutenga ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
Mpanzu, Chama, Oura jino kwa jino kuzifumania nyavu ligi kuu
1d ago
READ MORE β†’
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
Kapombe, Hamza, Nangu wamuongezea mzuka Barker
1d ago
READ MORE β†’