Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kufanya hafla ya utoaji wa Tuzo za Soka kwa msimu wa 2025/26 Desemba 12, 2026, jijini Arusha.
Tuzo hizo zitatambua mchango na mafanikio ya wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini katika msimu huo.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa, tuzo hizo zimegawanywa katika makundi matano ambayo ni Tuzo za Ligi Kuu ya NBC, Tuzo za Kombe la Shirikisho la CRDB, Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake, Tuzo za Ligi Nyingine na Tuzo za Utawala.
Kwa jumla, kutakuwa na vipengele 38 vya tuzo na watunukiwa 61. Msimu huu pia umeongezwa vipengele vitatu vipya ambavyo ni Mtanzania Anayecheza Nje kwa wanaume, Mtanzania Anayecheza Nje kwa wanawake na Kikundi Bora cha Ushangiliaji Uwanjani.
LIGI KUU YA NBC
Katika kundi la Ligi Kuu ya NBC, wachezaji na wadau mbalimbali wameingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za msimu wa 2025/26.
Mfungaji Bora
-
Nduhumwe Mosi (Singida BS)
Kipa Bora
-
Aishi Manula (Azam FC)
-
Djigui Diarra (Young Africans)
-
Mahamodou Kassali (Simba SC)
Beki Bora
-
Ibrahim Hamad (Young Africans)
-
Ibrahim Imoro (Singida BS)
-
Rushine De Reuck (Simba SC)
Kiungo Bora
-
Allan Okello (Young Africans)
-
Clatous Chama (Singida BS/Simba SC)
-
Feisal Salum (Azam FC)
-
Max Nzengeli (Young Africans)
-
Pacome Zouzoua (Young Africans)
Mchezaji Bora
-
Allan Okello (Young Africans)
-
Clatous Chama (Singida BS/Simba SC)
-
Feisal Salum (Azam FC)
-
Ibrahim Hamad (Young Africans)
-
Max Nzengeli (Young Africans)
-
Nduhumwe Mosi (Singida BS)
-
Pacome Zouzoua (Young Africans)
-
Rushine De Reuck (Simba SC)
Mchezaji Bora Chipukizi
-
Abdulkarim Kiswanya (Namungo FC)
-
Ashrafu Kibeku (Azam FC)
-
Juma Abushiri (Fountain Gate)
Kacha Bora
-
Etiene Ndayiraje (TRA United)
-
Florent Ibenge (Azam FC)
-
Steve Barker (Simba SC)
Kamishna Bora
-
Abousufian Silia (Iringa)
-
Hamis Kitila (Singida)
-
Osuri Kosuri (Simiyu)
Meneja Bora wa Uwanja
-
Jackson Mwendwa (Kwaraa, Manyara)
-
Omar Malule (Airtel, Singida)
-
Said Mpuche (Isamuhyo, Dar es Salaam)
Mwamuzi Bora
-
Ahmed Arajiga
-
Katanga Hussein
-
Sifu Amon
Mwamuzi Msaidizi Bora
-
Jesse Erasmo
-
Mohamed Mkono
-
Respicious Dismas
Seti Bora ya Waamuzi
-
Simba SC vs Pamba Jiji: Sifu Amon, Jesse Erasmo, Juma Said na Elly Sasii.
-
Azam FC vs Young Africans: Ahmed Arajiga, Mohamed Mkono, Rashid Zongo na Isihaka Mwalile.
-
JKT Tanzania vs Young Africans: Katanga Hussein, Makame Mdogo, Wema Kalinga na Alex Pancras.
Timu Yenye Nidhamu
-
Fountain Gate
-
KMC FC
-
Mbeya City
Aidha, washindi wa tuzo za Kikosi Bora cha Ligi Kuu, Goli Bora na Fair Play watatangazwa siku ya hafla.
KOMBE LA SHIRIKISHO LA CRDB
Katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, washindani wameingia kwenye vipengele vitatu vya tuzo.
Mchezaji Bora
-
Anicent Oura (Simba SC)
-
Clatous Chama (Simba SC)
-
Iddi Seleman (Azam FC)
Kipa Bora
-
Mamadou Kassali (Simba SC)
-
Metacha Mnata (Singida BS)
-
Zuberi Foba (Azam FC)
Mfungaji Bora
-
John Chinguku (Magnet FC)
TUZO ZA LIGI KUU YA WANAWAKE
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Wanawake, wachezaji, makocha na waamuzi wameingia kwenye orodha ya wanaowania tuzo mbalimbali.
Mchezaji Bora
-
Aisha Mnunka (Simba Queens)
-
Ester Maseke (JKT Queens)
-
Jamila Mnunduka (JKT Queens)
-
Jeannine Mukandayisenga (Yanga Princess)
-
Jentrix Shikangwa (Simba Queens)
Kipa Bora
-
Gelwa Yona (Mashujaa Queens)
-
Rita Akarekor (Yanga Princess)
-
Ruth Aturo (Simba Queens)
Mfungaji Bora
-
Jeannine Mukandayisenga (Yanga Princess)
Kocha Bora
-
Edna Lema (Yanga Princess)
-
Juma Kessy (JKT Queens)
-
Mussa Mgosi (Simba Queens)
Mchezaji Bora Chipukizi
-
Bahati Kizanguzi (Bunda Queens)
-
Elizabeth Mwiti (Simba Queens)
-
Jamila Athumani (Tausi FC)
Timu Yenye Nidhamu
-
Alliance Girls
-
Ceasiaa Queens
-
Simba Queens
Mwamuzi Bora
-
Anitha Kisoma
-
Monica Wazael
-
Tatu Malogo
Mwamuzi Msaidizi Bora
-
Maria Mwakitalima
-
Sikudhani Mkurungwa
-
Zawadi Yusuph
Kikosi Bora cha Ligi Kuu ya Wanawake pia kitatangazwa wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo.
TUZO ZA LIGI NYINGINE
Katika kundi la ligi nyingine, kutakuwa na tuzo kwa wachezaji wanaoshiriki NBC Championship, First League na Ligi ya NBC U-20.
Mchezaji Bora NBC Championship
-
Denis Mushi (Polisi Tanzania)
-
Maulid Juma (Geita FC)
-
Obrey Chirwa (Kagera Sugar)
Mchezaji Bora First League
-
Ally Mwinjuma (NKIM FC)
-
Danford Kaswa (Bandari Tanzania)
-
George Komba (Rhino Rangers)
Mchezaji Bora Ligi ya NBC U-20
-
Abdallah Mkude (Azam FC)
-
Mahsen Saleh (Young Africans)
-
Said Nkondo (JKT Tanzania)
WATANZANIA WANAOCHEZA NJE YA NCHI
Moja ya mambo mapya katika tuzo za msimu huu ni kuanzishwa kwa vipengele vya kuwatambua Watanzania wanaofanya vizuri katika klabu za nje ya nchi, kwa upande wa wanaume na wanawake.
Mtanzania Anayecheza Nje – Wanaume
-
Alphonce Mabulla (FC Shamakhi, Azerbaijan)
-
Charles M'mombwa (Floriana FC, Malta)
-
Haji Mnoga (Salford City, England)
-
Mbwana Samatta (Le Havre, Ufaransa)
-
Novatus Miroshi (Göztepe FC, Uturuki)
Mtanzania Anayecheza Nje – Wanawake
-
Clara Luvanga (Al-Nassr, Saudi Arabia)
-
Diana Lucas (Trabzonspor, Uturuki)
-
Hasnath Ubamba (FC Masar, Misri)
-
Julitha Singano (Juárez FC, Mexico)
-
Opa Clement (SD Eibar, Hispania)
TUZO ZA UTAWALA
Katika kundi la Tuzo za Utawala, kutakuwa na vipengele vitano ambavyo washindi wake watatangazwa wakati wa hafla hiyo.
-
Tuzo ya Rais.
-
Tuzo ya Heshima.
-
Tuzo ya Heshima Soka la Wanawake.
-
Tuzo ya Mchezaji Gwiji.
-
Tuzo ya Kikundi Bora cha Ushangiliaji Uwanjani.