Mkurugenzi wa ufundi wa Simba, Honour Janza, ameeleza kuwa ni heshima na fursa ya kipekee kuteuliwa kushika wadhifa huo ndani ya klabu hiyo yenye historia kubwa na mafanikio makubwa nchini na barani Afrika.
Kupitia mahojiano yake na Simba TV, Janza ameishukuru bodi na menejimenti ya klabu kwa imani kubwa waliyoionyesha kwake na kumpa nafasi hiyo adhimu.
"Ni heshima kubwa kwangu kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa Simba, hii ni klabu yenye historia kubwa barani Afrika na hapa nchini, na kila mwanasoka angependa kuwa sehemu ya historia yake. Namshukuru Mungu kwa nafasi hii adimu ya kuwa sehemu ya historia ya Simba," alisema.
Janza tayari ameanza rasmi majukumu yake ndani ya Simba juzi akikutana kwa mara ya kwanza na benchi a ufundi linaloongozwa na kocha Steve Barker.
Janza atafanya kazi kwa ukaribu na Barker katika maboresho ya timu na kuhakikisha Simba inaendelea kufanya vyema na kufikia malengoo yake.


