Baada ya mapumziko ya wiki moja, kikosi cha Simba kimerejea rasmi mazoezini Mo Simba Arena kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.
Nyota wote ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wameripoti Mo Simba Arena leo kwa ajili ya maandalizi hayo.
Pamoja na malengo ya kuendeleza kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi, mwishoni mwa mwezi Simba inaanza rasmi kampeni ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya Orlando Pirates.
Simba imepangwa kundi C ikiwa pamoja na RS Berkane, Orlando na Colombe Fc.












ADVERTISE HERE