Sakata la kisheria baina ya vinara wa ligi kuu ya NBC Simba SC na Kocha Mkuu wa Yanga SC, Fadlu Davids, halikunza leo kwani kesi hiyo ilifunguliwa tangu mwaka jana.
Wakati huu imepangwa rasmi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuanza kusikilizwa mwezi Januari 2027.
Mzozo huo unatokana na madai ya Simba SC dhidi ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini, wakimtuhumu kwa kuvunja mkataba kinyume na taratibu wakati wa kipindi chake cha kuhudumu ndani ya klabu hiyo.
Simba imefungua madai ya fidia ya kifedha baada ya Fadlu Davids kuondoka kambini nchini Botswana bila kibali maalum cha uongozi, kufuatia mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United msimu uliopita.
Kutokana na kitendo hicho, Idara ya Sheria ya Simba, chini ya Mwanasheria wake Hosea Chamba, iliwasilisha shauri rasmi mbele ya vyombo vya maamuzi vya FIFA ili kupata fidia na haki zao za kimkataba.