Barker afafanua mapumziko ya wachezaji, apania kuendeleza ubabe baada ya FIFA break

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3h ago
Barker afafanua mapumziko ya wachezaji, apania kuendeleza ubabe baada ya FIFA break

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema anaamini muda wa mapumziko aliyowapa wachezaji wake unatosha kurejesha miili yao katika hali bora kabla ya kuendelea na maandalizi kuelekea mechi zinazofuata ligi kuu na ligi ya mabingwa.

Baada ya ushindi wa mbao 3-2 dhidi ya Namungo Fc, Barker alitoa wiki moja kwa wachezaji wake kumpumzika ambapo kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kinatarajiwa kurejea mazoezini siku ya Jumatatu.

“Mapumziko haya ni muhimu kwetu kwa sababu yanatupa nafasi ya kuangalia tulipotoka na tunakokwenda."

"Tunataka kutumia muda huu kufanya kazi kwenye maeneo yanayohitaji maboresho, kuhakikisha wachezaji wanakuwa katika hali nzuri na tunarejea tukiwa tayari kwa changamoto zinazotukabili. Tunajua michezo ijayo haitakuwa rahisi, hivyo tunahitaji maandalizi bora,” alisema Barker

Kwa mujibu wa ratiba, mchezo unaofuata wa Simba ni dhidi ya JKT Tanzania ukiwa ni wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Isamuhyo, Novemba 21.

Baada ya mchezo huo, Simba itaelekeza nguvu zake kwenye ligi ya mabingwa hatua ya makundi ikitarajiwa kuanza na Orlando Pirates nyumbani.

Barker atakuwa na takribani siku 10 za kukiweka sawa kikosi chake tayari kwa awamu nyingine ya ushindani Simba ikilenga kuendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kurudi Uhuru CAFCL, ni baada ya CAF kuidhinisha
Simba kurudi Uhuru CAFCL, ni baada ya CAF kuidhinisha
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
12h ago
READ MORE β†’
TFF yaweka hadharani ratiba ya uchaguzi Simba
TFF yaweka hadharani ratiba ya uchaguzi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Hapo kwenye asisti Gueye ameshindikana
Hapo kwenye asisti Gueye ameshindikana
1d ago
READ MORE β†’
Kuna rekodi ya maisha Barker anaiweka Msimbazi
Kuna rekodi ya maisha Barker anaiweka Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Ratiba ya Simba kufunga mwaka 2026
Ratiba ya Simba kufunga mwaka 2026
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
1d ago
READ MORE β†’
Nindi ana walimu wazuri Simba, atakuwa beki bora
Nindi ana walimu wazuri Simba, atakuwa beki bora
2d ago
READ MORE β†’
Barker, Mpanzu watwaa tuzo za ligi kuu Oktoba 2026
Barker, Mpanzu watwaa tuzo za ligi kuu Oktoba 2026
2d ago
READ MORE β†’
Wachezaji Simba wapewa mapumziko, kurejea Novemba 09
Wachezaji Simba wapewa mapumziko, kurejea Novemba 09
2d ago
READ MORE β†’