Baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa leo kwenye uwanja wa Uhuru, ligi inatarajiwa kusimama kwa takribani wiki tatu kupisha kalenda ya FIFA.
Inaelezwa uongozi wa Simba chini ya Rais wa heshima Bilionea Mohamed Dewji 'Mo', umepanga kuipeleka timu Kenya kuweka kambi ya maandalizi kuelekea mechi za hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.
Kwa mujibu wa ratiba mechi za hatua ya makundi CAFCL zinatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu Simba ikiwa kundi C pamoja na RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe ya Cameroon.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Simba kuweka kambi nje ya nchi wakati wa mapumziko ya FIFA.
Walifanya hivyo mwishoni mwa Septemba na waliporejea waliendeleza wimbi la ushindi kwenye ligi ikiwa ni pamoja na kuwatandika wapinzani wao wakuu Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu.