Wagombea waanza kurejesha fomu Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Sep 2018
Wagombea waanza kurejesha fomu Simba
Wakati kikosi chake kikijiandaa kwa mchezo wao wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC, upande wa pili wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa timu hiyo umefikia patamu kufuatia jumla ya wanachama 21 kujitokeza kuchukua fomu.

Wanachama hao jana walianza kuzirudisha fomu hizo baada ya kuzijaza ambapo mchakato huo utaenda hadi Jumamosi.

Akizungumza jana, Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Steven Ally, alisema hadi mchakato huo wa uchukuaji fomu unafungwa jumla ya wanachama 21 walikuwa wamechukua fomu, huku Swedi Mkwabi na Mtemi Ramadhani wakijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa bodi wa klabu hiyo.

"Tunashukuru zoezi la kuchukua fomu tumelifunga... wanachama 21 wamejitokeza, sasa tunasubiri wazirejeshe ili taratibu nyingine ziendelee," alisema Ally.

Alifafanua kuwa wajumbe wanaotakiwa kutoka upande wa wanachama ni nane ambapo sita watakuwa wa kuchaguliwa na wawili wa kuteuliwa na kati yao lazima kuwe na mjumbe mwanamke.

Katika wanachama waliochukua fomu kuwania uongozi, Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah 'Try Again' hakujitokeza.

Uchaguzi huo wa Simba umepangwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu, huku kamati ikisisitiza katiba itakayotumika ni ile ya toleo la mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho na kuingiza mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika hatua nyingine, nyota wa Simba waliokuwa kwenye majukumu na timu zao za taifa wanaanza kurejea leo kuungana na wenzao kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.

Nyota wa Simba waliokuwa kwenye majukumu ya timu za taifa ni Aishi Manula (Taifa Stars) ambaye yeye tayari ameungana na timu, huku wanaosubiriwa ni Meddie Kagere (Rwanda), Emmanuel Okwi na Juuko Mursheed (Uganda) pamoja na kiungo Cletus Chama kutoka Zambia.

Simba yenye pointi sita baada ya kushuka dimbani mara mbili msimu huu, itavaana na Ndanda FC Jumamosi kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’