TFF yaingilia kati uchaguzi SImba 'mchakato lazima uendelee'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2h ago
TFF yaingilia kati uchaguzi SImba 'mchakato lazima uendelee'

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kusimamia moja kwa moja mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba SC baada ya kubaini mapungufu katika ratiba na utaratibu wa uchaguzi uliotangazwa awali na klabu hiyo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa kuzingatia Katiba ya klabu, kanuni za uchaguzi pamoja na taratibu zinazotakiwa kisheria.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kiburu Kibamba, amesema uamuzi huo umefikiwa kufuatia kamati yake kupokea malalamiko kuhusu utaratibu uliotumiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company katika kuandaa mchakato wa uchaguzi.

Kwa mujibu wa Kibamba, kamati ilipokea barua mbili kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF. Barua ya kwanza ilihusu taarifa ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa Simba SC, huku barua ya pili ikiwa na malalamiko kuhusu utaratibu uliotumiwa na bodi hiyo.

Kutokana na malalamiko hayo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliamua kuwaita na kuwasikiliza wahusika wa pande zote kabla ya kutoa maelekezo kuhusu namna mchakato huo utakavyoendelea.

Kibamba ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo walikutana na wawakilishi wa pande mbili zinazohusika, akiwamo Crescentius Magori aliyewakilisha upande wa mwekezaji na Murtaza Mangungu aliyewakilisha upande wa wanachama.

Hata hivyo Kibamba amesema kutokana na mapungufu waliyoyabaini kwenye ratiba ya uchaguzi iliyotolewa awali, watahitaji kuiboresha ratiba hiyo kabla ya kutangaza mchakato sahihi kuelekea uchaguzi huo.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Matola atahadharisha mechi dhidi ya Namungo Fc, mkakati ni alama tatu
Matola atahadharisha mechi dhidi ya Namungo Fc, mkakati ni alama tatu
2h ago
READ MORE β†’
Simba vs Namungo Fc; Ahmed awaalika mashabiki dimba la Uhuru
Simba vs Namungo Fc; Ahmed awaalika mashabiki dimba la Uhuru
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mligo, Chilambo wajumuishwa kikosi cha Stars
Mligo, Chilambo wajumuishwa kikosi cha Stars
1d ago
READ MORE β†’
Namungo Fc wanatafuta kipigo kizito kutoka kwa Simba
Namungo Fc wanatafuta kipigo kizito kutoka kwa Simba
1d ago
READ MORE β†’
Simba haipaswi kuruhusu kivuli cha migogoro wakati huu wa dhahabu
Simba haipaswi kuruhusu kivuli cha migogoro wakati huu wa dhahabu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
1d ago
READ MORE β†’
Simba yarejea Dar kituo kinachofuata ni Namungo Fc
Simba yarejea Dar kituo kinachofuata ni Namungo Fc
1d ago
READ MORE β†’
Alama tatu kwenye nyakati ngumu ni matokeo mazuri - Barker
Alama tatu kwenye nyakati ngumu ni matokeo mazuri - Barker
2d ago
READ MORE β†’
Simba ni mwendo wa rekodi msimu huu
Simba ni mwendo wa rekodi msimu huu
2d ago
READ MORE β†’