Namungo Fc wanatafuta kipigo kizito kutoka kwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Namungo Fc wanatafuta kipigo kizito kutoka kwa Simba

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC na Namungo FC, klabu ya Namungo imetuma ujumbe mzito kwa Wekundu wa Msimbazi kupitia barua ya wazi iliyochapishwa na klabu hiyo.

Kupitia barua hiyo yenye kichwa cha habari “Barua kwa Simba”, Namungo FC imeeleza kusikitishwa na taarifa za malalamiko kutoka kwa baadhi ya timu ndogo zilizokutana na Simba kabla ya mchezo wao.

Namungo imeeleza kuwa imeamua kulibeba suala hilo na kulifanya kuwa jambo la kitaifa, huku ikiahidi kuhakikisha inatoa kipigo kwa Simba ili iwe fundisho.

Katika sehemu ya barua hiyo, Namungo imeandika:

“Wauaji wa Kusini tumelibeba swala hili na kuwa jambo la kitaifa, hivyo tutahakikisha tunawapiga kipigo cha paka mwizi ili iwe fundisho.”

Ni wazi huu ni uchokozi wa waziwazi! Simba SC itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri ya mwanzo wa msimu, ikiwa imeshinda michezo yote tisa ya awali na kuendelea kushikilia nafasi ya kileleni mwa msimamo wa ligi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumatatu, Novemba 02, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa Namungo FC.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mligo, Chilambo wajumuishwa kikosi cha Stars
Mligo, Chilambo wajumuishwa kikosi cha Stars
24m ago
READ MORE β†’
Simba haipaswi kuruhusu kivuli cha migogoro wakati huu wa dhahabu
Simba haipaswi kuruhusu kivuli cha migogoro wakati huu wa dhahabu
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
8h ago
READ MORE β†’
Simba yarejea Dar kituo kinachofuata ni Namungo Fc
Simba yarejea Dar kituo kinachofuata ni Namungo Fc
19h ago
READ MORE β†’
Alama tatu kwenye nyakati ngumu ni matokeo mazuri - Barker
Alama tatu kwenye nyakati ngumu ni matokeo mazuri - Barker
1d ago
READ MORE β†’
Simba ni mwendo wa rekodi msimu huu
Simba ni mwendo wa rekodi msimu huu
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Fountain Gate 0-1 Simba (FT)
Highlights; Fountain Gate 0-1 Simba (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1d ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
1d ago
READ MORE β†’
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
1d ago
READ MORE β†’