Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amekiri kuwa kikosi chake hakikuonyesha kiwango bora kinachotarajiwa kwenye ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa jana.
Hata hivyo Barker amesisitiza kuwa jambo la msingi zaidi lilikuwa ni kuondoka na alama tatu muhimu na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
Akizungumza mara baada ya mtanange huo, Barker alibainisha kuwa suala la uchovu uliotokana na ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo ziliathiri timu yake, lakini akafurahishwa na namna wachezaji walivyopambana kiume kulinda ushindi huo.
"Hukuwa mchezo mzuri sana kwetu. Tulikuwa chini ya kiwango chetu cha kawaida leo, na lazima nikiri Fountain Gate walitupa upinzani mkubwa. Hata hivyo, kwenye mbio hizi za ubingwa, mechi za ugenini kama hizi huwa ngumu sana. Kitu cha muhimu zaidi ilikuwa ni kupata alama tatu, na vijana wamepigana hadi sekunde ya mwisho kuzilinda," alisema Barker.
Ushindi huo umeifanya Simba SC kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa tofauti ya alama tano wakiendeleza rekodi ya ushindi wa asilimia 100 msimu huu.